Orodha ya mwisho ya wachezaji watatu kutoka barani Afrika, wanaocheza soka katika ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1, wanaowania tuzo ya mwaka 2025/2026 ya Marc-Vivien Foé inayotolewa na RFI-France 24 imewekwa wazi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watatu hao ni pamoja na Lamine Camara, mwenye umri wa miaka 22, kiungo wa kati wa klabu ya Monaco. Camara ni raia wa Senegal.

Raia mwenzake Moussa Niakhaté, mwenye umri wa miaka 30, beki anayecheza katika klabu ya Lyon, pia ametajwa katika orodha hii ya mwisho.

Kiungo wa Kati Mamadou Sangaré, mwenye umri wa miaka 23, anayecheza katika klabu ya Lens, raia wa Mali pia anawania tuzo hiyo.

Mshindi wa tuzo hii anatarajiwa kutangazwa siku ya Jumatatu, Mei tarehe 11.

Tangu mwaka 2011, tuzo hii imekuwa ikitolewa kwa mchezaji bora kutoka barani Afrika, anayeza soka nchini Ufaransa kumuenzi na kumkumbuka Marc-Vivien Foé, aliyekuwa mchezaji wa Cameroon, aliyepoteza maisha Juni tarehe 26 mwaka 2003 kwenye uwanja wa Gerland jijini Lyon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *