
Nchini Ivory Coast, serikali imetangaza kuvunjwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, iliyoundwa mwaka 2001, ambapo tangu kipindi hicho, imekuwa ikiandaa na kusimamia uchaguzi mbalimbali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imekuja baada ya Tume hiyo kushuhudia ukosoaji mkubwa kutoka kwa vyama mbalimbali vya siasa, tangu mwaka 2010 wakati nchi hiyo ilipoingia kwenye mzozo wa kisiasa, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakiishtumu Tume hiyo kwa kuupendelea muungano unaotawala, madai ambayo imekuwa ikikanusha.
Msemaji wa serikali Amadou Coulibaly, amesema, hatua hiyo iliafikiwa ili kuwepo na mfumo mpya wa usimamizi wa uchaguzi na kusaidia kurejesha imani ya umma katika mchakato mzima wa uchaguzi katika nchi hiyo.
Aidha, amesema kuwa majadiliano yanaendelea kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuunda Tume mpya.
Ivory Coast ilikuwa uchaguzi wa urais mara ya mwisho Oktoba mwaka uliopita , ambapo Rais Alassane Ouattara alishinda muhula wa nne kwa karibia asilimia 90, katika uchaguzi uliosusiwa na viongozi waandamizi wa upinzani.