Rais wa Marekani Donald Trump anadai kwamba usitishaji mapigano na Iran bado unaendelea licha ya shambulio la meli tatu za kivita za Marekani mapema siku Alhamisi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mvutano kati ya Marekani na Iran umeongezeka tena baada ya pande hizo mbili kurushiana mashambulizi saa 24 zilizopita, katika tukio linalotajwa kuwa jaribio kubwa zaidi kwa sitisho la vita lililodumu kwa mwezi mmoja.

Akizungumza mjini Washington, Trump alipunguza uzito wa tukio hilo akisema, “Walitujaribu leo, nasi tukawajibu vikali,” huku akisisitiza kuwa sitisho la vita bado lipo. Marekani pia ilikuwa ikisubiri majibu ya Iran kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano bila kutatua moja kwa moja suala la mpango wa nyuklia wa Iran.

“Wamecheza nasi leo. Tumewashinda. Wamecheza. “Naita hilo kuwa ni jambo dogo,” rais wa Marekani amewaambia waandishi wa habari. Mapigano haya yanakuja huku Washington bado ikisubiri jibu kutoka Tehran kwa pendekezo lake la hivi karibuni la usitishaji mapigano wa kudumu.

kwa Upande wake, Iran imedai kushambulia meli za kijeshi za Marekani karibu na bandari ya Chabahar kujibu mashambulizi ya Marekani dhdi ya meli zake mbili karibu na Mlango bahari wa Hormuz pamoja na maeneo ya raia katika kisiwa cha Qeshm na pwani ya kusini mwa Iran.

Wakati huo huo Shirika la kimataifa la masuala ya bahari la Umoja wa Mataifa (IMO) limesema takribani meli 1,500 pamoja na mabaharia zaidi ya 20,000 wamekwama katika eneo la Ghuba ya Uajemi kutokana na vikwazo vya Iran kwenye njia ya Mlango wa Hormuz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *