Nchini Msumbiji, akiba ya mafuta haitoshi tena. Serikali ya Daniel Chapo sasa inalazimika kuongeza bei. Serikali ilisita kutekeleza hatua hii isiyopendwa na raia baada ya ghasia za hivi karibuni za baada ya uchaguzi, lakini hatimaye imekubali kuetekeleza kutokana uhaba na foleni ndefu katika vituo vya mafuta.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mauzo ya mafuta hayakuwawezesha tena wasambazaji kufidia gharama zao. Mafuta yaliyoagizwa yamekuwa ghali sana, na kuuza tena kwa bei iliyowekwa na serikali hakukuwa na faida tena. Ili kutoa shinikizo, baadhi ya vituo vya mafuta vilizuia usambazaji kwa kutarajia ongezeko la bei.

Hii ni athari ya tatizo la mafuta linlosababishwa na kuzingirwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

Tangu kuanza kwa vita nchini Iran, mafuta yamepanda bei kutoka takriban dola 60 hadi dola 100 kwa pipa.

Msumbiji inalenga kukuza uwezo wake wa ndani wa kusafisha mafuta ili kupunguza utegemezi wake kwa mafuta yanayoagizwa kutoka nje na kuimarisha usalama wake wa nishati. Mamlaka imeona mradi huo kuwa “wa dharura.” Nchi hiyo haiko peke yake katika kuongeza bei; nchini Ethiopia, Zambia, na Gambia, bei ya mafuta iliongezeka kwa hadi 26% wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *