Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns ambako mataifa hayo yamekubaliana kushirikiana katika utafiti wa madini.

Akizungunza katika mkutano huo waziri Mavunde amebainisha kuwa moja ya kipaumbele kikuu cha sekta ya madini ni utafiti ambao utasaidia kutambua aina na kiwango cha rasilimali madini tulizobarikiwa nchini kwetu na kuvutia uwekezaji.

“Tunafamu kuwa nchi yetu imefanya utafiti wa kina wa kurusha ndege kwa asilimia 16 tu. Hivyo, tuna uhitaji mkubwa wa kupata uwekezaji zaidi katika eneo hili ili kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye maendeleo yete.”

Kwa mujibu wa waziri Mavunde, nchi yetu imeigawanywa katika bloku sita ambapo mpaka sasa bloku moja pekee ipo mbioni kuanza kufanyiwa utafiti kupitia mradi unatakaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia Serikali ya Spain hivyo bad funa fursa kwa zilizobaki.

Kwa upande wake, balozi Burns ameshukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwake na kueleza utayari wa Kampuni kutoka nchini Canada kuja kuwekeza nchini Tanzania.

Balozi Burns amesema anafurahishwa na namna Tanzania tunavyosimamia shughuli za uchimbaji mdogo na kusisitiza kuwa Canada ipo tayari kuyaleta makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya uchimbaji hususan uchenjuaji madini ili viweze kusaidia kuongeza tija kwa wachimbaji wadogo nchini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *