Senegal inashughulikia tatizo la baadhi ya wabunge ambao wanasusia vikao vya Bunge bila sababu za msingi. Siku ya Ijumaa, Mei 8, 2026, Bunge, linalotawaliwa na chama tawala cha PASTEF, lilipitisha muswada huo kwa kura 127 dhidi ya 3, huku wabunge 2 wakikijizuia kupiga kura. Muswada huo unafafanua na kuimarisha vikwazo dhidi ya wabunge waliochaguliwa wanaojihusisha na tabia ya kususia bunge.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Ibara ya 118 ya sheria za utaratibu wa Bunge tayari imetoa nafasi ya kusitishwa kwa posho za bunge (na uwezekano wa kutimuliwa kwenye nafasi hiyo) kwa mbunge ambaye ataonekana kuendelea kususia vikao vya bunge mara kwa mara na bila sababu. Lakini kwa Ayib Daffé, kiongozi wa kundi la wabunge wa chama tawala cha PASTEF, ibara hiyo, ambayo haitumiki sana, inastahili ufafanuzi: “Bado ilikuwa muhimu kutoa vikwazo vya mwisho kwa kuanzia na onyo rasmi. Onyo rasmi huanza na kutoshiiki mara nne kwenye kikao kisichokuwa cha kawaida cha Bunge bila udhuru wowote. Na hata kabla ya maonyo rasmi na adhabu za kifedha, unaombwa kujieleza kuhusu kutokuwepo kwako katika kikao cha Bunge. Kwa hivyo, nadhani kuna ulinzi wa kutosha ili kuwaruhusu wabunge kufanya kazi yao ipasavyo.”

“Hili sio tatizo linalozuia Bunge kufanya kazi.” Na baada ya kutoshiriki vikao vya Bunge mara kumi bila sababu, mbunge hupoteza kiti chake. Kwa Cheikh Ahmed Tidiane Youm, mbunge wa chama cha upinzani cha PUR, Bunge halina mamlaka ya kubatilisha mamlaka ya mbunge, na hakuna haja ya sheria kushughulikia kutoshiriki katika vikao vya Bunge mara kwa mara, kulingana naye: “Ni tatizo la kisiasa. Ninawakilisha kundi la wabunge, nina mbunge ambaye hashiriki vikao vya Bunge, Ni jukumu langu kumuonya na kumuweka sawa. Kwa nini kuweka sheria? Ni tatizo la kisiasa linalohitaji kutatuliwa kisiasa.”

Thierno Alassane Sall, mbunge mwingine wa upinzani, ambaye alipiga kura dhidi ya sheria hiyo, ambayo anaiona kuwa inalenga kujenga chuki dhidi ya wabunge wengine. Anasema Senegal ina vipaumbele vingine: “Wakati wa kikao hiki cha kutunga sheria, hatujapata tatizo la akidi. Kwa hivyo si suala hili linalozuia Bunge kufanya kazi. Masuala muhimu zaidi hayajadiliwi, kama vile kiwango cha sasa cha deni na sera zinazotekelezwa ili kutusaidia kutoka katika hali hii.”

“Tunatunga sheria kwa kipaumbele,” anajibu Ayib Daffé wa Pastef.

Kufikia sasa haijawezekana kujua kutoka kwa Bunge ni wabunge wangapi kati ya 165 ambao hususia vikao vya Bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *