SERIKALI inatarajia kuzindua mpango mkakati wa mageuzi ya mazingira endelevu (2026–2030) unaolenga kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamadi Yussuf Masauni, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa mpango huo ni sehemu ya mageuzi mapana ya sekta ya mazingira yanayolenga kushughulikia changamoto mbalimbali, zikiwemo usimamizi duni wa taka ngumu mijini, matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali, pamoja na uharibifu wa mazingira.

Masauni amesema mkakati huo ni mfumo wa kitaifa wa mwongozo utakaoratibu hatua za kimazingira kwa kipindi cha miaka mitano.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *