Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5
Labda kama umeruka darasa la elimu ya masuala ya kujamiian, pengine una ufahamu wa kimsingi jinsi watoto wanavyoumbwa.
Yai lazima lirutubishwe na manii wakati wa dirisha maalum la mzunguko wa hedhi ili maisha yaanze.
Kujamiiana hutoa hali bora kwa uzazi. Lakini hiyo haina maana kwamba ujauzito wowote hutokea kwa njia hii.
Pia kuna mifano ya wanawake wanaopata ujauzito katika njia mabzo ni nadra sana kutokea ambayzo mtu anaweza kufikiria kuwa haiwezekani.
1. Kupitia njia ya haja kubwa
Ingawa visa vya ujauzito unaotokana na ngono ya njia ya haja kubwa ni nadra sana, lakini hutokea. Hata hivyo, visa hivyo vimetokea tu kwa watu wenye hitilafu ya mfumo wa uzazi inayojulikana kama ‘cloacal malformation’.
Tatizo hili hutokea kwa msichana mmoja kati ya 50,000 na linahitaji uingiliaji wa upasuaji wa kurekebisha.
Hata hivyo, hata baada ya hayo, kuna uwezekano mkubwa kwamba itasababisha matatizo kama vile figo kushindwa kufanya kazi, kushindwa kujizuia, ugumu wa kupata mimba, na kuongezeka kwa hatari ya kuzaliwa kabla ya wakati.
Chanzo cha picha, Getty Images
Cloaca ni “uwazi wa kawaida” wa njia ya mkojo, kujisaidia haja kubwa, na kujifungua. Ni kawaida kuzingatiwa katika wanyama wanaotambaa, ndege, na hata platypus.
Kwa wanaume, tishu ambayo hukua chini na kugawanya cloaca katika maeneo mawili au tatu, kulingana na jinsia. Lakini katika hali nadra, tishu hii inashindwa kutenganisha kabisa rectum (njia ya haja kubwa) kutoka kwa cavity ya uke.
Hili linapotokea, mbegu za kiume zinaweza kuogelea kupitia uwazi wowote kwenye ukuta wa seli hadi kwenye yai ili kulirutubisha. Kisha yai lililorutubishwa litapandikizwa kwenye uterasi kama kawaida.
Ikiwa unashangaa kwa nini mbegu za kiume haziendelei kusafiri hadi kwenye rektamu, ni kwa sababu zinafanya kazi kupitia kemotaksi. Hii inamaanisha zinaweza kugundua athari za kemikali zinazozalishwa na yai.
Mbegu zinapoogelea kuelekea kwenye yai, kiasi cha “chemoattractants” hizi wanazogundua huongezeka, na kuwaambia waendelee kusafiri katika mwelekeo sahihi.
2. Kupitia njia ya mdomo
Uwezo thabiti wa manii kufikia yai labda unaonyeshwa zaidi kuliko hapo awali katika mojawapo ya matukio ya ajabu zaidi yaliyorekodiwa katika maandiko ya matibabu.
Mwanamke aliyezaliwa bila uke alikwenda kwa daktari akilalamikia maumivu ya mara kwa mara ya tumbo ambayo, kwa njia nyingi, huiga mikazo.
Uchunguzi zaidi wa madaktari ulibaini kuwa kulikuwa na kijusi ndani ya tumbo lake la uzazi na kwamba uchungu wa mwanamke huyo ulitokana na kwamba alikuwa katika leba.
Mtoto alizaliwa mara moja kwa njia ya upasuaji.
Chanzo cha picha, Getty Images
3. Mimba za Splash
“Splash pregnancy” ni njia nyingine ya mtu kupata mimba bila kujamiiana. Hii ni mimba inayosababishwa na mbegu za kiume kumwagika karibu na uke bila kufanya tendo la ndoa rasmi.
Kama jina lake linavyopendekeza, ikiwa manii yatamwagika kwenye sehemu ya siri ya nje, inaweza kufika kwenye uke na mbegu kuogelea hadi kwenye ovari.
Aina hii ya ujauzito ni ngumu sana kutokea lakini inatajwa, kwani manii hayaishi zaidi ya nusu saa nje ya mwili. Wakati manii yenye afya huogelea kwa kasi ya hadi 5 mm kwa dakika, huishi tu kwa muda mdogo (hadi siku tano katika viungo vya uzazi wa kike).
Chanzo cha picha, Getty Images
Kati ya mamia ya mamilioni ya mbegu za kiume zinaingia kwenye uke wakati wa kujamiiana, ambapo katika hali nzuri, ni 200 hadi 300 tu hufikia yai. Ni rahisi kuelewa kwa nini mimba zisizopangwa ni nadra sana.
Mimba haiwezi kusababishwa na kunyunyiza manii wakati wa kuoga, kwa sababu maji hutawanya manii na hupunguza unyevunyevu ambao kwa kawaida hulinda manii kutoka kwa viungo vya ndani vya uzazi vya mwanamke na ulimwengu wa nje.
Kemikali kama klorini katika maji pia huua mbegu za kiume haraka.
4. Mimba ya mapacha
Mwili una utaratibu za kuzuia mimba kutokea wakati mwanamke tayari ni mjamzito.
Hii ni kweli hata kwa wanawake waliozaliwa na uterasi mbili, kwa sababu taratibu hizi hufanya kazi kwa bidii ili kuzuia mimba ya pili.
Homoni hizo huzuia kudondoshwa kwa yai na kutoa ute mnene unaofunika seviksi ili kuzuia manii kupita kwenye uterasi hadi kwenye ovari.
Lakini jambo, linaloitwa superfetation, hutupilia mbali sheria hizi nje ya dirisha.
Utaratibu huu husababisha mimba ya pili kudhihirika huku ile ya kwanza ikiwa tayari inaendelea.
Ni jambo nadra sana kwamba wanasayansi hawaelewi jinsi inavyotokea. Visa vingi vilivyorekodiwa vilihusisha wanawake ambao walikuwa wamepitia utungaji mimba wa vitro.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kawaida, mimba hizo mbili hutokea katika muda mfupi sana, zikiwa na pengo la wiki mbili hadi nne kati ya kwanza na ya pili. Hii ina maana kwamba watoto wanaweza kuzaliwa wakati mmoja, kama mapacha.
Ingawa kuna tofauti katika umri wa mimba, nyingi kati ya mimba hizi huendelea kama kawaida bila matatizo mengine zaidi ya yale yanayojulikana sana.
Bila shaka, matukio ya namna hii ni nadra sana, hivyo huenda usihitaji kuwa na wasiwasi mkubwa. Hata hivyo, ikiwa huna mpango wa kupata mimba hivi karibuni, hakikisha unatumia njia ya uzazi wa mpango.
Haya ni kwa mujibu wa Adam Taylor, profesa na mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Anatomia ya Kitabibu (Clinical Anatomy Learning Centre) katika Chuo Kikuu cha Lancaster, Uingereza.