Kundi la waasi wa AFC/M23 – linaloungwa mkono na Rwanda – limejiondoa kutoka maeneo kadhaa huko Kivu Kusini, mashariki mwa DRC. Kujiondoa huku kufuatia shinikizo kutoka kwa Marekani, wapatanishi katika mzozo kati ya DRC na kuni hili la waasi. Marekani ilikuwa imewataka wapiganaji wa AFC/M23 wajiondoe hadi takriban kilomita 70 kaskazini mwa jiji la Uvira, ambalo lilitekwa na M23 mnamo mwezi Desemba 2025.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashahidi, wapiganaji wa M23 walianza kujiondoa jioni ya Jumapili, Mei 10, 2026. Wakiwa Sange na takriban kilomita 30 kaskazini mwa Uvira tangu walipoondoka katika mji wa Uvira katikati ya mwezi Januari, wanaendelea kujiondoa kuelekea kaskazini kando ya barabara ya Uvira/Bukavu.

Sange, Nyakabere, Luberizi, Bwegera… Kujiondoa kwao kumethibitishwa na jeshi la Kongo, ambalo baadaye lilitangaza kurejea kwao katika maeneo haya katika Uwanda wa Ruzizi na Nyanda za Juu. Hata hivyo, kwa upande wa kundi hilo lenye silaha hawazungumzii kama kujiondoa, bali kama “kujipanga upya.” “Hili ni tendo la nia njema, kulingana na mchakato wa amani,” afisa mkuu wa AFC/M23 amesema.

Kurudi kwenye ngome zao za mwishoni mwa mwaka 2025

Ikumbukwe kwamba kitendo cha wasi wa AFC/M23 cha kukamata mji wa Uvira mnamo mwezi Desemba 2025 kiliikasirisha Washington, ambayo ilidai kujiondoa upande mmoja. Kulingana na jeshi la Kongo, AFC/M23 sasa imerejea Luvungi, kilomita 65 kaskazini mwa Uvira. “Tunarudi kwenye nafasi zetu kutoka kabla ya kukamatwa kwa Uvira,” chanzo cha usalama ndani ya kundi hilo lenye silaha kimebainisha.

Siku ya Ijumaa, Mei 8, 2026, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa wito kwa pande zinazopigana kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano na kupunguza mvutano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *