
Angalau watu tisa wameuawa na takriban kumi wametekwa nyara katika shambulio jipya la kundi la jihadi la ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na takwimu za mashirika ya kiraia. Kundi hilo lenye silaha lililenga mji wa Makumo katika eneo la Mambasa mkoani Ituri. Eneo hili tayari lilikumbwa na shambulio kama hilo mapema wiki iliyopita, ambalo pia linahusishwa na ADF.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi
Wasiwasi uliendelea kuripotiwa Makumo siku ya Jumatatu, siku moja baada ya shambulio hili la hivi karibuni la kundi la ADF. Shughuli zilizorota, na wakazi walisita kurudi kwenye mashamba yao.