Ziara ya Nick Checker, afisa kutoka Ofisi ya Masuala ya Afrika ya Marekani katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, mnamo Mei 7 na 8, 2026,  imetoa fursa ya kutoa ujumbe muhimu. Ahadi zilizovunjwa za Juba kuhusu uwekezaji katika huduma za msingi kwa wakazi wake, kukamatwa na kushtakiwa kwa Makamu wa Rais Riek Machar…

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Juba, Florence Miettaux

Washington inazitaka pande hasimu katika mgogoro wa nchi hiyo kurudi kwenye mkataba wa amani wa mwaka 2018, ambao umekuwa ukikiukwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, huku kukiwa na mapigano mapya.

Taarifa za Nick Checker kufuatia mkutano wake na maafisa wa serikali ya Sudan Kusini, ambao majina yao hayajawekwa wazi, zinakuja katika wakati mbaya kwa kambi ya Salva Kiir. Washirika wa rais wa Sudan Kusini wanajaribu kuushawishi umma kwamba wanataka kufanya uchaguzi mnamomwezi  Desemba 2026, na kwamba kwa lengo hili, mazungumzo ya kisiasa yanaendelea na upinzani. Mkuu mpya wa jeshi hata alitangaza siku ya Jumatatu kuunganishwa kwa makundi ya upinzani katika jeshi la Sudan Kusini.

“Ujanja”

Lakini Nick Checker hakushawishika waziwazi, akitangaza: “Ni ujanja kudai kwamba mazungumzo kati ya vyama yanaendelea wakati Makamu wa Rais Riek Machar, ambaye anaongoza chama cha pili kwa ukubwa katika makubaliano ya mwaka 2018, uyko kizuizini na ameshtakiwa.” Afisa huyo wa Marekani aliendelea kuwashutumu viongozi wa Sudan Kusini kwa “kutumia vibaya migogoro ambayo wao wenyewe wameisababisha na ahadi za uongo za mageuzi na maandalizi ya uchaguzi kama njia ya kuomba msaada wa kimataifa.”

Siku ya Jumatatu Bunge la taifa lilikumbwa na mvutano unaoendelea kati ya wafuasi wa Riek Machar na wale wa Salva Kiir: Wabunge watiifu kwa makamu wa rais waliondoka wakati wa kikao cha Bunge wakipinga nia ya kambi ya rais ya kupitisha marekebisho ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018 kwa njia “isiyojumuisha wote”, wakipuuza taratibu zilizotolewa katika mkataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *