Serikali mkoani Ruvuma inatarajiwa kunufaika na miradi 57 ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, maji na miundombinu. Miradi hiyo ina thamani ya zaidi ya Sh bilioni 21.7 na itapitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 katika halmashauri nane za mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo.
(Feed generated with FetchRSS)