
Pentagon imetathmini upya gharama ya vita nchini Iran hadi sasa kwa karibu dola bilioni 29 za Marekani, afisa mkuu wa anayehusika na masuala ya fedha ametangaza siku ya Jumanne wakati wa kikao kipya cha bunge, pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiasi hiki ni karibu dola bilioni 4 zaidi ya makadirio yaliyowasilishwa wiki mbili zilizopita wakati wa mkutano uliopita na wabunge wa Marekani, ambapo ilikuwa mara ya kwanza mkuu wa Pentagon anahojiwa bungeni tangu kuanza kwa vita mwishoni mwa mwezi Februari.
Wakati huo, makadirio yalikuwa dola bilioni 25. Lakini makao makuu ya jeshi la Marekani na Mdhibiti Mkuu wanapitia makadirio hayo kila mara, na sasa tunaamini yanakaribia dola bilioni 29, alielezea afisa mkuu wa masuala ya fedha jeshi Jules Hurst, ambaye aliambatana na Pete Hegseth na Mkuu wa jeshi, Jenerali Dan Caine.
Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Tehran mnamo Februari 28.
Mpango wa kusitisha mapigano umekuwepo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na mazungumzo kati ya Washington na Tehran yanayolenga kukomesha vita vya Mashariki ya Kati yamekwama.