
Maeneo ya Kusini mwa nchi ya Somalia, yako hatarin kukumbwa na njaa ambapo wilaya moja imeripoti kiwango cha juu cha njaa ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu mwaka 2022, yamesema mashirika mawili yakimataifa yanayofuatilia mwenendo wa usalama wa chakula duniani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwaka 2011, Somalia, moja ya mataifa yenye uhaba mkubwa wa chakula duniani kutokana na ukame, migogoro na umaskini, ilikumbwa na njaa, ambapo takriban watu laki 2 na elfu 50 walikufa.
Katika kipindi hiki, kupungua kwa misaada ya nje na athari za vita ya Marekani na Iran, vimesababisha sintofahamu zaidi ya juhudi za kukabiliana na upungufu wa chakula kulikochangiwa na ukosefu wa mvua mara kwa mara na utovu wa usalama unaoendelea kuripotiwa.
Mashirika hayo yanasema zaidi ya asilimia 37 ya watoto kwenye wilaya ya Burhakaba iliyoko kusini mwa nchi hiyo, wanasumbuliwa na utapiamlo na hali huenda ikawa mbaya zaidi ikiwa misaada itapunguzwa zaidi.
Mkurugenzi wa shirika la msaada la Mercy Corps nchini humo, Daud Jiran, amesema Somalia iko katika hatari ya kukabiliwa na mojawapo ya majanga makubwa zaidi duniani wakati huu mahitaji yanaongezeka na bei za bidhaa ikiendelea kupanda.