
Chama cha kiongozi wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, FATAH, hivi leo kitachagua viongozi wapya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10, wakati huu kikikabiliwa na wakati mgumu kutokana na mzozo wa Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kufuatia kikao cha siku tatu kilichoanza juma hili, vuguvugu hilo litachagua viongozi wa kamati kuu licha ya kupoteza umaarufu wake kutokana na serikali ya Abbas kutuhumiwa kwa vitendo vya rushwa na kasi ndogo ya kufanikisha uhuru wa eneo hilo.
Kamati itakayochaguliwa inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mustakabali wa eneo hilo ikiwa Abbas mwenye umri wa miaka 90 hivi sasa ataamua kuachia ngazi.
Kwa muda Fatah imekuwa kiungo muhimu kwa utawala wa PLO, ambapo wanaungwa mkono na raia wengi wa Palestina, hata hivyo wakilitenga Kundi la Hamas, ambalo lilipata umashuhuri mkubwa kwenye eneo la ukingo wa magharibi katika uchaguzi wa mwaka 2006.
Akihutubia wafuasi wake, Abbas amesema yuko tayari kutekeleza mabadiliko ya kiuongozi ikiwa ni pamoja na kuandaa uchaguzi wa rais na wabunge ambao haujafanyika kwa zaidi ya muongo mmoja.