“Sisi Wenyeviti wa ACT Wazalendo wa Mikoa 11 ya Kichama Zanzibar tunatoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuiweka hadharani rpoti yote ya Tume ya Jaji Chande. Hii itasaidia kuelewa kwa kina mbinu za kiuchunguzi za Tume na matokeo ya uchunguzi huo.

“Muhtasari wa taarifa
uliosomwa na Jaji Chande umeacha maswali mengi kuliko majibu. Ingawa Tume ya Jaji Chande ni ya Rais kama ambavyo Rais Samia amesema, lakini suala ambalo ilipewa ilichunguze ni suala zito lenye maslahi mapana ya Taifa. Watanzania wana haki ya kujua kwa kina kile ambacho Tume ya Jaji Chande imekwishawasilisha”Haji Dude Haji, Mwenyekiti wa Mkoa wa Kichama wa Mjini kwa niaba ya Wenyeviti wa Mikoa yote 11 ya ACT Wazalendo Zanzibar.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *