Shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, limesema waasi wa M23 na vikosi vya wanajeshi wa Rwanda, walitekeleza vitendo vya kihalifu kwa zaidi ya mwezi mmoja wakati walipovamia mji wa Uvira, mashariki mwa nchi ya DRC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch, katika ripoti yake iliyochapisha Alhamisi hii, imesema askari hao walibaka wanawake na wasichana, kutekeleza mauaji ya pamoja na kuwapoteza mamia ya raia.

Shirika hilo linasema limerekodi matukio 50 ya mauaji ya kupangwa na angalau matukio 8 ya ubakaji na mengine ya ufyatuliaji risasi raia waliokuwa wanakimbia mapigano.

Ripoti ya shirika hilo imeongeza kuwa, wapiganaji wa M23 pamoja na wanajeshi wa Rwanda, walipita nyumba kwa nyumba na kuwalenga wanaume na wavulana waliotuhumiwa kushirikiana na wapiganaji Wazalendo.

Human Rights Watch imesema iliwasiliana na Serikali ya Rwanda na kiongozi wa waasi hao, Betrand Bisimwa kutaka kupata sehemu ya utetezi wao, hata hivyo hawakujibiwa, shirika hilo likitoa wito wa uchunguzi huru.

Machi 2 mwaka huu, Serikali ya Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya jeshi la Rwanda Pamoja na maofisa wake wa juu kwa madai ya kuwasaidia waasi wa M23 kutatiza usalama mashariki mwa Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *