Zaidi ya watu milioni 26.5 nchini DRC wanakabiliwa na uhaba wa chakula, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa—sawa na Mkongo mmoja kati ya Wakongo wanne.Mpango wa msaada kwa sasa haufadhiliwi kikamilifu, laonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo mawili yanatoa tahadhari kuhusu mgogoro huu wa chakula, “mojawapo ya mizozo mikubwa zaidi duniani.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi

“Huu ni mgogoro uliojikita zaidi,” linasema Shirika la Chakula Duniani, “unaowaweka mamilioni ya kaya zilizo hatarini katika mzunguko wa uhitaji unaoendelea.” Uhaba huu wa chakula unaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa nchini DRC.

Kulingana na data kutoka Uainishaji Jumuishi wa Awamu ya Usalama wa Chakula (IPC), iliyochapishwa katika taarifa ya pamoja siku ya Jumatano, Mei 13, 2026, zaidi ya watoto milioni 4 walio chini ya umri wa miaka mitano “watahitaji matibabu ya utapiamlo mkali” kati ya ” mwezi Januari na Juni 2026.” Miongoni mwao, zaidi ya milioni 1.3 wanakabiliwa na au wako katika hatari ya kupata utapiamlo mkali, hali ambayo inaweza “kuua ndani ya wiki chache bila matibabu ya haraka,” mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yamesema.

Mpango wa usaidizi unahitaji ufadhili zaidi

Zaidi ya wanawake wajawazito au wanaonyonyesha milioni 1.5 pia wanatarajiwa kuathiriwa na utapiamlo huu mkali, na kuzidisha hatari za kiafya kwa akina mama na watoto. Maisha ya karibu Wakongo milioni 3.6 yanatishiwa moja kwa moja na mgogoro huu wa chakula.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) leo wamesema waziwazi kwamba hawana rasilimali. WFP inakadiria upungufu huo kuwa dola milioni 214 hadi mwezi Oktoba. FAO, kwa upande wake, inaomba haraka dola milioni 163 ili kusaidia msimu wa kilimo kabla ya msimu ujao wa kupanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *