Uwanja mpya wa Yanga unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 24, baada ya kutangazwa rasmi kwa kuanza kwa mradi huo katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Ijumaa Mei 15, 2026 katika hafla ya utiaji saini wa mradi huo, Rais wa Yanga, Hersi Said, amesema ujenzi wa uwanja huo utaongeza hadhi ya klabu hiyo na kuwa alama mpya ya maendeleo ya michezo nchini.

“Ndugu Wanayanga, hivi karibuni klabu yenu itakuwa na uwanja hapa katika eneo hili (Jangwani). Mungu akijaalia ‘maximum’ miezi 18 mpaka 24 tutasimama hapa kuzindua uwanja huu wa kisasa,” amesema Hersi.

Hersi amesema mradi wa ujenzi wa uwanja huo utawafanya kumiliki asilimia 50 huku mwekezaji ambaye ni Kampuni ya GSM akimiliki kiasi hicho pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *