Kiongozi wa Wachache wa Seneti ya Marekani: Safari ya Trump nchini China Ilikuwa fedheha tupuKiongozi wa Wachache wa Seneti ya Marekani: Safari ya Trump nchini China Ilikuwa fedheha tupu

Chuck Schumer, Kiongozi wa Wachache katika Seneti ya Marekani, amesema kwamba safari ya Rais Donald Trump nchini China haikuwa na mafanikio yoyote kwa watu wa Marekani na ilikuwa fedheha kamili.

Chuck Schumer ameandika katika ujumbe wake kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X, akiashiria safari ya Rais wa Marekani nchini China kwamba: “Safari hii, ambayo ilifanywa kwa taratibu zote za kiprotokali, haikuwa na mafanikio yoyote kwa watu wa Marekani kuhusu ushuru, biashara, Mlango Bahari wa Hormuz, vita vya Asia Magharibi au vita vya Ukraine. Ilikuwa kashfa kamili na aibu tupu na halisi.”

Kiongozi wa Wachache wa Chama cha Democratic katika Seneti ya Marekani pia amezungumzia kufeli kwa Trump katika siasa za ndani, akisisitiza: “Hana ufanisi vilevile nje ya nchi, na kitu pekee anacholeta nyumbani ni kwamba Rais wa China, Xi Jinping, amemkemea kuhusu suala la Taiwan.”

Rais wa Marekani Donald Trump alikamilisha safari yake ya siku tatu nchini China siku ya Ijumaa na kuondoka Beijing akirejea Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *