Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Kuhusu “Siku ya Nakbat”; Uhalifu wa Israel ni jinai ya kivitaTaarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Kuhusu “Siku ya Nakbat”; Uhalifu wa Israel ni jinai ya kivita

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza katika taarifa iliyotolewa kwa mnasaba wa tukio la “Siku ya Nakbat” kwamba uhalifu unaofanywa na Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina ni kielelezo halisi cha jinai za kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari, na kwa msingi huu, mahakama za kimataifa zinataka kuwaadhibu wahalifu wa Kizayuni.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kwamba: Katika kumbukumbu ya kuanzishwa uwepo wa utawala wa Kizayuni katika eneo la Asia Magharibi na dunia kwa ujumla, ambayo inaitwa kwa haki Siku ya Nakbat, (Siku ya Maafa) Iran inasisitiza haki ya watu wa Palestina kuamua hatima yao wenyewe, na inaikumbusha jamii ya kimataifa kuhusu wajibu wake wa kisheria na kimaadili wa kukomesha mauaji ya kimbari, uvamizi na kujaribu kuwaadhibu wahalifu Wazayuni.

Miaka 78 iliyopita, katika siku hii, janga baya zaidi la binadamu na la kimaadili la zama za sasa lilitokea kwa kutangazwa kuanzishwa utawala bandia wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya kihistoria ya Palestina, ambalo matokeo yake mabaya yanaonekana katika eneo la Asia Magharibi na kote duniani.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema: “Siku ya Nakba ni ukumbusho wa njama za maadui wa binadamu dhidi ya Palestina na eneo la Asia Magharibi, ambalo matokeo yake ya moja kwa moja yamekuwa ukosefu wa usalama wa kudumu katika eneo hilo na kuhalalishwa uvunjaji sheria na uhalifu.

Imesema: “Katika miongo hii minane, ukiukwaji mkubwa zaidi wa sheria za kimataifa umefanywa na Wazayuni wavamizi, kwa msaada wa Marekani, Uingereza, Ujerumani, Canada na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya, katika Palestina inayokaliwa. Katika miaka mitatu iliyopita, mpango wa kikoloni wa kuiangamiza Palestina umeingia katika awamu mpya, na utawala ghasibu umefanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina kwa kutumia silaha hatari zaidi zilizotolewa na Marekani na waungaji mkono wake wa Magharibi.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeeleza katika taarifa hiyo kwamba: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na watu huru duniani, inalaani vikali uhalifu wa utawala wa Kizayuni, ikisisitiza haki ya msingi ya watu wa Palestina kupambana na uvamizi na ubaguzi wa rangi, na inapinga kikamilifu mpango wowote unaohusisha kuhamishwa kwa mabavu watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi kutoka kwenye nchi yao.”

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kusisitiza msimamo wake thabiti wa kuunga mkono haki halali ya watu wa Palestina ya kupambana na uvamizi na uchokozi, haki ya wakimbizi wa Palestina kurudi katika nchi yao, na kuanzishwa taifa huru na lenye umoja la Palestina mji mkuu wake mkuu ukiwa al Quds (Jerusalem).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *