
Nchini Chad, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anatoa wito kwa mamlaka ya Chad na Nigeria kufanya “uchunguzi wa haraka, wa kina, huru, na usioegemea upande wowote” kufuatia mashambulizi ya mabomu yaliyosababisha vifo siku ya Jumapili, Mei 10, 2026, kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambayo yanaripotiwa kuua raia kadhaa. Umoja wa Mataifa unahusisha mashambulizi hayo na majeshi ya Nigeria na Chad, ambayo yanadai kuwa yanawasaka wanamgambo wa Boko Haram.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu mwanzoni mwa mwezi Mei, mashambulizi ya Boko Haram yameongezeka katika eneo la Ziwa Chad, na kusababisha vifo vya raia na wanajeshi, anaripoti mwandishi wetu huko N’Djamena, Nadia Ben Mahfoudh.
Siku ya Ijumaa, Mei 8, 2026, jeshi la Chad lilitangaza kuwa lilifanya operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Boko Haram na yaliendesha mashambulizi ya mambomu ili kuwaondoa na kuwaangamiza watu hao wanaohusishwa kuwa wa kundi hilo. Serikali ya Chad ilithibitisha kuwa ilikuwa ikiendesha operesheni hiyo na jeshi la Nigeria.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa siku ya Jumatano, Mei 13, 2026, Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, alisema “ameshtushwa na kusikitishwa” na idadi ya vifo vya raia vilivyosababishwa na mashambulizi ya anga ya ndege za kivita za Chad, ambazo alisema zililenga visiwa vilivyotengwa kaskazini mashariki mwa Nigeria. Ingawa visiwa hivi vinajulikana kuwa na kambi za Boko Haram, Umoja wa Mataifa uliripoti vifo vya takriban raia zaidi ya mia moja, hasa wavuvi wa Nigeria.
Mamlaka inadai kila wakati kwamba “raia wameokolewa”
Serikali ya Chad, kupitia msemaji wake, inasema iko wazi kwa uchunguzi wa kimataifa na inakanusha madai hayo. “”Tuna tuna uwezo na vyombo ili kutofautisha Boko Haram na raia. Tumehakikisha kila mara kwamba raia wanaokolewa; hakuna raia aliyefariki katika mashambulizi haya,” alisema Gassim Chérif Mahamat, Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali, kwa vyombo vya habari nchini Chad siku ya Alhamisi.
Kwa upande wake, jeshi la Nigeria lilisema kwamba lililenga “kundi la magaidi lililothibitishwa, ambalo lilikuwa tishio la moja kwa moja kwa maisha ya raia.”
Uwanda huu mkubwa wa maji katikati ya Sahel, pamoja na visiwa vyake vingi ambavyo ni vigumu kufikiwa, umebadilisha eneo hilo kuwa ngome ya wanajihadi. Wapiganaji kutoka kundi la Boko Haram na ISWAP wamekuwa wakiendesha harakati zao katika eneo hilo kwa karibu miaka 20. Na mashambulizi ya kujibu kutoka majeshi ya Chad na Nigeria yanashutumiwa mara kwa mara kwa kusababisha vifo vingi vya raia.
