Jiongeze: Harmo wa Kajala na Marioo wa Paula Jiongeze: Harmo wa Kajala na Marioo wa Paula 

Dar es Salaam. Utulivu ni mkubwa kwa Marioo kukaa kando ya Paula. Na Paula amebadilika sana baada ya ujio wa Marioo kwenye maisha yake. Tofauti ni kubwa ukilinganisha na ‘wazazi’ wao Konde na Kajala.

Waswahili wana msemo kwamba “anayelala na mama yako huyo ni baba yako.” Kwa maana hiyo ni sawa tukisema wazazi wa Paula na Marioo. Kimsingi Konde Boy ni mkwe wa Marioo mbali na P Funk. 

Kabla ya Marioo kuutunza moyo wa Paula. Binti yule alikuwa na mambo mengi ambayo kwa sasa yametoweka. Marioo hata kabla ya Paula hakuwa na vurugu sana. Lakini thamani yake imepaa sana kwa sasa baada ya uwepo wake kwa Paula.

Kuna ‘klipu’ imesambaa ya Konde akimwagia pesa Sallam. Kwenye sherehe ya kuzaliwa ya Mendez. Ukiutazama uso wa Sallam huoni kama anafurahia kitendo kile. Na hata Konde haoneshi kama ana ‘lavu’ na anachofanya.

Kimsingi ni pigo za ‘kiwaki’ sana. Pigo hizo hufanywa kwenye ‘ishu’ za kibao kata na dadazi. Kule sio ‘kushoo lavu’ ni ‘kushoo ofu’ kitu kinacholeta tofauti na nyakati na umri. Hakuna mabadiliko kwenye ubongo wa Konde.

Wakati watoto wao wanabadilika na kutulia. Wazazi wameshindwa kubadilika. Kuna namna wakati ule Kajala alimbadilisha Konde hata kwenye mikato ya pamba. Tulitegemea hata sasa mambo yangebadilika. 

Penzi la kijana kwa mtu mzima, husaidia mabadiliko ya kitabia. ‘Shoo ofu’ za pesa ni ushamba kama ushamba mwingine. Siyo vibaya wazazi hawa wakajifunza kwa watoto Marioo na Paula. Ni wazi watoto wametulia kuliko wazazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *