
Dar es Salaam. Wakati dunia ikisubiri kwa hamu kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia 2026, kampuni ya ubashiri ya Leonbet imezindua kampeni maalum yenye lengo la kuongeza msisimko kwa mashabiki wa soka kuelekea mashindano hayo makubwa duniani.
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika kwa mara ya kwanza katika mataifa matatu ambayo ni Canada, Marekani na Mexico, huku pia zikiweka rekodi mpya ya kushirikisha timu 48 badala ya 32 zilizokuwa zikishiriki hapo awali.
Katika kuelekea mashindano hayo, Leonbet imekuja na kampeni mpya itakayowapa washiriki nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo gari aina ya Mazda CX-3, safari ya kifahari kwenda Ngorongoro, PlayStation 5 (PS5), simu ya iPhone 17 Pro Max pamoja na fedha taslimu.
Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, kampeni hiyo ilianza Mei mwaka huu na itahitimishwa Julai 19, 2026 sambamba na mwisho wa mashindano ya Kombe la Dunia.
Washiriki wa kampeni hiyo watatakiwa kuweka dau kupitia tovuti au programu rasmi ya Leonbet kwa kiwango cha kuanzia Sh3,000 ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye droo zitakazochezeshwa katika hatua mbalimbali za mashindano hayo kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Leonbet, Jérôme Dufourg, amesema lengo kuu ni kuongeza burudani kwa mashabiki wa soka wakati wa Kombe la Dunia huku wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
“Kampeni hii inalenga kuongeza msisimko wa Kombe la Dunia 2026 na kuwapa mashabiki nafasi ya kushinda zawadi kubwa wakati wakifuatilia michezo,” amesema Dufourg.
Kwa upande wake, balozi wa Leonbet, Baraka Mpenja, amesema kampuni hiyo inaendelea kuboresha huduma zake kwa lengo la kuwapa Watanzania nafasi zaidi za kushiriki michezo ya ubashiri na kujishindia zawadi.
“Leonbet imeendelea kuboresha huduma zake na kutoa nafasi kwa mashabiki kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali kupitia kampeni tofauti,” amesema Mpenja.
