Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa imelaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Israel dhidi ya wafungwa wa Kipalestina, ikitaka kufanyike uchunguzi huru, usioegemea upande wowote na wa wazi kuhusu visa vyote vya vifo, mateso, unyanyasaji na ukiukaji mwingine, na kwa wale waliohusika kuwajibishwa.

Msemaji wa tume hiyo, Thamin Al-Khitan, amesema kwamba wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israel wanakabiliwa na mateso na unyanyasaji wa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na kijinsia, akieleza kuwa suala hili linajumuisha visa vingi vya ubakaji, ikiwa ni pamoja na wa kuwaba watoto.
Matamshi ya Al-Khitan yametolewa kufuatia ripoti ya mwandishi habari wa New York Times, Nicholas Kristof, ambayo imefichua kwamba wafungwa wa Kipalestina, wakiwemo watoto, walibakwa kimfumo na kushambuliwa kingono na wanajeshi wa Israel, walowezi wa Kizayuni na walinzi wa magereza.
Al-Khitan amethibitisha kwamba tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imethibitisha vifo vya wafungwa wapatao 90 wa Kipalestina waliokuwa kizuizini huko Israel tangu Oktoba 7, 2023, ikibainisha kuwa mmoja wa waathiriwa alikuwa mvulana wa miaka 17 ambaye alipatikana na dalili za njaa kali wakati wa kifo chake.
Ripoti ya New York Times, ambayo imeikasirisha Israel, ilijumuisha ushuhuda kutoka kwa wafungwa 14 wa zamani wa Kipalestina waliozungumzia unyanyasaji na mashambulizi ya kutisha ya kingono dhidi ya wafungwa wa Kipalestina.