Watu wenye silaha wawateka nyara makumi ya wanafunzi katika Jimbo la Borno nchini NigeriaWatu wenye silaha wawateka nyara makumi ya wanafunzi katika Jimbo la Borno nchini Nigeria

Watu waliokuwa na silaha wameteka nyara makumi ya wanafunzi wa shule katika jimbo lililokumbwa na machafuko la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wanamgambo hao walivamia Shule ya Msingi na Sekondari ya Mussa katika eneo la Serikali ya Mtaa la Askira-Uba saa tatu asubuhi siku ya Ijumaa wakati masomo yakiendelea na kuwachukua wanafunzi kadhaa na kuondokana nao. Haya yameelezwa na Ubaidallah Hasaan, mkazi wa karibu na shule hiyo, alipozungumza na shirika la habari la Reuters.

Wakati huo huo mwalimu wa shule hiyo ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hao waliokuwa na silaha walifika shuleni kwa kutumia pikipiki. “Licha ya wanafunzi wengine kutorokea vichakani, lakini naweza kuema wengi walitekwa nyara na wahalifu hao,” amesema mwalimu wa shule ya msingi na sekondari ya Mussa katika jimbo la Borno, Nigeria.

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na utekaji nyara huo ambapo kundi la Boko Haram linashukiwa kuhusika. Mbunge wa eneo la Midala, Usman Balami amelitaja shambulizi hilo kuwa la “kuvunja moyo” na kuitaka mamlaka husika kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *