Chipukizi United yazipigia hesabu mechi za nyumbaniChipukizi United yazipigia hesabu mechi za nyumbani

Chipukizi United baada ya kuvuna alama tatu ugenini, sasa inarejea nyumbani kisiwani Pemba kujiandaa ya michezo  minne ya kukamilisha msimu wa 2025-2026 ndani ya Ligi Kuu Zanzibar.

Chipukizi ilikuwa Unguja kucheza mechi mbili za ligi hiyo na ilipoteza dhidi ya Mafunzo kwa mabao 2-1, kisha ikashinda 3-2 mbele ya Kipanga.

Timu hiyo hadi kufikia sasa haijajihakikisha kusalia Ligi Kuu Zanzibar kwa sababu ya alama ilizokuwa nazo 34, baada ya kucheza mechi 26 ikiwa nafasi ya 10.

CHIPU 01

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa timu hiyo, Kheri Kidema amesema mikakati yao ilikuwa ni kushinda mechi zote mbili lakini mambo mengine yamewaendea vibaya.

Kidema amesema hawawezi kushuka daraja kwa sababu wana kikosi imara na wanarudi kujipanga kwa ajili ya michezo minne ya nyumbani iliyobaki, lengo likiwa ni kuchukua alama zote 12 ili kuwa salama. “Msimu huu malengo yetu yalikuwa ni kuwa mabingwa au kumaliza ndani ya nne bora, lakini tulianza ligi vibaya, naamini msimu ujao tutakuwa imara.” amesema Kidema.

CHIPU 02

Kiongozi huyo aliongeza, wamebakisha mechi nne ambazo zote ni ngumu dhidi ya Polisi, Mlandege, KMKM na JKU na wakishinda tatu, basi watakuwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *