Ebola Ituri: WHO na WFP watoa tani 5 za vifaa vya kukabiliana na EbolaEbola Ituri: WHO na WFP watoa tani 5 za vifaa vya kukabiliana na Ebola

Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamepeleka tani 5 za vifaa huko Bunia siku ya Jumapili, Mei 17, 2026, kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti mlipuko wa Ebola katika mkoa wa Ituri.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa yalileta “ndege iliyobeba tani 5 za vifaa kwa ajili ya majibu ya awali. Vifaa hivi ni pamoja na aproni, glavu, barakoa, na kofia, ili kuwalinda wafanyakazi wa afya kutokana na maambukizi na kuwazuia kusambaza virusi kwa raia,” alielezea Anne Ancia, Mwakilishi wa WHO nchini DRC.

Kwa vifaa hivyo kuna klorini na vifaa vya kusafisha vizuri vituo vya afya pia viliwasilishwa.

Kumepangwa kuanzisha “miundombinu ya afya kwa ajili kuhudumia wagonjwa. Tumeleta mahema, magodoro, vitanda,” alisema Anne Ancia.

Timu za wataalamu

Kulingana na Anne Ancia, wataalamu wa afya zaidi ya arobaini, wataalamu kutoka Kituo cha Operesheni za Dharura huko Kinshasa na timu kutoka Shirika la Afya Duniani pia zimetumwa katika eneo hilo. Lengo la uingiliaji kati huu ni kuimarisha huduma kwa wagonjwa na kuokoa maisha ya raia.

WHO pia inatoa wito kwa wakazi kuunga mkono juhudi za Serikali na washirika wake, hasa kwa kurahisisha utambuzi wa watu waliotngamana na wagonjwa walioambukizwa virusi vya Ebola  ili kudhibiti mlipuko huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *