Iran yasema mazungumzo kati yake na Marekani yanaendeleaIran yasema mazungumzo kati yake na Marekani yanaendelea

Iran kupitia Wizara yake ya Mambo ya nje, imesema mazungumzo na Marekani yanaendelea kupitia Pakistan ambaye ni mpatanishi kwa lengo la kupata mkataba wa kudumu, ili kumaliza vita vya Mashariki ya Kati.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Mambo ya nje wa Iran Esmaeil Baqaei, amesema tayari Iran imeshajibu, mapendekezo 14 kupitia Pakistan, yaliyopendekezwa na Marekani kama njia za kumaliza vita na kupatikana kwa mkataba wa amani.

Wakati mazungumzo hayo yakiripotiwa kuendelea, rais wa Marekani Donald Trump, ameonya Iran kuwa muda unakwenda sana, kuhusu upatikanaji wa mkataba huo wa amani licha ya vyombo vya Habari vya Iran kuripotiwa kuwa mapendekezo ya Iran, hayatekelezi.

Katika hatua nyingine, baraza la juu la usalama nchini Iran, limetangaza kuundwa kwa kundi jipya la watalaam wa usalama, kusimamia mlango wa Bahari wa Hormuz.

Hii inakuja baada ya washirika wa Marekani kama Saudi Arabia na Falme za Kiarabu kushambuliwa na ndege zisizokuwa na rubani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *