
Raia wa Kenya, hivi leo wamepata wakati mgumu kufika kwenye maeneo yao ya kazi kufuatia mgomo uliotangazwa na wamiliki wa mabasi ya abiria na bodaboda unaoanza hivi leo kushinikiza serikali kushusha bei ya mafuta.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Aidha wadau wanataka kuvunjiliwa mbali kwa mamlaka ya udhibiti wa nishati na mafuta, EPRA.
Kulingana na wawakilishi katika sekta ya uchukuzi wa umma, serikali imeendelea kuongeza bei ya mafuta bila kujali raia wa kawaida, hali ambayo wanasema imewafanya Wakenya kukabiliwa na kipindi kigumu cha maisha.
Kando na uchukuzi wa umma, sekta ya utali na ile ya usafirishaji wa mizigo pia inatarajiwa kuathirika, waratibu wa mgomo huu wakisisitiza kuwa ni lazima serikali ipunguze bei ya mafuta iliotangazwa Mei 14.
Mgomo wa leo unakuja baada ya wahudumu wa uchukuzi wa umma kutangaza kuongeza nauli kwa asilimia 50.
Kwa sasa lita moja ya petroli jijjni Nairobi inauzwa kwa shilling 214.25 wakati diseli ikiiuzwa kwa shilling 242.92, Hadi tukiandaa ripoti hii, magari ya usafiri wa umma hayakuwa yanatoa huduma kama kawaida.
