Somalia: Karibu watu milioni sita wako hatarini kutokana na ukosefu wa usalama wa chakulaSomalia: Karibu watu milioni sita wako hatarini kutokana na ukosefu wa usalama wa chakula

Nchini Somalia, baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), shirika lisilo la kiserikali la Mercy Corps sasa linaibua wasiwasi kuhusu hali ya njaa ambayo inaweza kuathiri karibu watu milioni 7. Nchi hiyo ina idadi ya watu milioni 15. Mchanganyiko wa mambo—ukosefu wa mvua, vita nchini Iran, na kupungua kwa misaada ya kimataifa—unaathiri moja kwa moja nchi hiyo, ambayo iko “katika kipindi kigumu,” kulingana na shirika la misaada la Marekani nchini Somalia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Somalia, maeneo yote ya vijijini nchini yameathiriwa na mgogoro huu wa chakula, karibu 70%  ya nchi hiyo, linabaini shirika lisilo la kisetrikali la Marekani la Mercy Corps. Mgogoro huu umezidishwa na mgogoro katika Mashariki ya Kati, ambao unaongeza bei, na msimu mbaya wa mvua, anasema Daud Jiran, mkurugenzi wa shirika la Mercy Corps nchini Somalia.

“Hali ni mbaya zaidi kwa sababu mvua imekuwa ndogo sana hivi karibuni.” Msimu mkuu wa mvua nchini ulikuwa mbaya, na inakadiriwa kuwa karibu watu milioni 6.5 sasa wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Kwa kupungua kwa misaada ya kimataifa, “sio tu kuhusu kuishi, bali ni hali ya maisha au kifo”

Mercy Corps pia inalaani kupungua kwa misaada ya kimataifa, ambayo imesababisha kumalizika kwa misheni kadhaa za dharura nchini Somalia. Daud Jiran anazungumzia hali ya maisha kwa familia nyingi.

“Familia nyingi sasa zinawasili katika kambi za watu waliokimbia makazi yao, kwa hivyo si tu kuhusu kuishi, bali ni hali ya maisha au kifo. Tunatumai kwamba jumuiya ya kimataifa itafikiria hili na kutoa msaada wa haraka.”

Shirika la Mercy Corps linakumbusha kwamba mnamo mwaka 2011, kuchelewa kwa mwitikio wa kibinadamu kulisababisha mgogoro ambao haujawahi kutokea. Kulingana na makadirio ya shirika hili, watu 250,000 walipoteza maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *