
Mshauri mkuu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema kwamba mkono wa chuma wa vikosi vya jeshi na taifa thabiti la Iran vitailazimisha Marekani kurudi nyuma na kusalimu amri.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X, Mohsen Rezaei, kamanda mkuu wa zamani wa Jeshi wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), amekejeli mbinu ya Washington isiyo thabiti na ya woga.
Rezaei ameandika kwamba Rais wa Marekani, Donald Trump, “huweka tarehe ya mwisho ya shambulio la kijeshi na kisha kulifuta mwenyewe, kwa maturajio yasiyo na maana ya kulilazimisha taifa na maafisa wa Iran kujisalimisha!”
“Nguvu ya chuma ya vikosi vyenye nguvu na taifa kubwa la Iran itailazimisha Marekani kurudi nyuma na kusalimu amri,” ameongeza Mohsen Rezaei.
Matamshi ya Rezaei yametolewa baada ya Trump kutangaza Jumatatu kwamba ameahirisha shambulio kubwa la kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, ambalo amedai lilikuwa limepangwa kufanyika Jumanne.
Akitetea kurudi nyuma kwake, Trump amedai “Tamim bin Hamad Al Thani, Emir wa Qatar, Mohammed bin Salman Al Saud, Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia na Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Falme za Kiarabu, wameniomba niahirishe shambulio letu la kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwani mazungumzo mazito yanaendelea.”
Trump ameongeza: “Kwa maoni yao, kama viongozi na washirika wakubwa, makubaliano yatafikiwa ambayo yatakubalika sana kwa Marekani, pamoja na nchi zote za Asia Magharibi na zaidi.”
Tangu kuanza kwa vita dhidi ya Iran, Trump ameanisha tarehe tano tofauti za mwisho za kutimizwa matakwa yake, na katika kila hatua, amelazimika kurudi nyuma na kutupilia mbali vitisho vyake kwa visingizio kadhaa, saa chache kabla ya tarehe ya mwisho, baada ya Iran kumpuuza maneno yake.
