
Nchini Sudan, Abu Lu Lu, kamanda mkuu wa vikosi vya wanamgambo wa RSF, ambaye alipewa jina la utani la mchinjaji wa El-Fasher, amerudi mstari wa mbele. Kamanda huyu wa FSR aliyezaliwa al-Fateh Abdullah Idriss, alikamatwa na kambi yake manmo mwezi Oktoba mwaka uliyopita, akituhumiwa kuwaua raia wengi wakati wa kukamatwa kwa El-Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Abu Lu Lu alipaswa kushtakiwa na wakubwa wake. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilimwekea vikwazo. Lakini kulingana na shirika la habari la REUTERS, ameachiliwa na inasemekana amerudi katika uwaja wa vita.
Abu Lou Lou alijulikana kwa kujirekodi wakati wa kukamatwa kwa mji wa El-Fasher, akiwaaibisha raia kabla ya kuwaua. Video zake, zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii, zilizua hasira kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hadi wakubwa wake kuchukuwa hatua ya kumkamata kamanda huyo na kuahidi kumfikisha mahakamani.
Wanamgambo wa RSF pia walirusha video inayomuonyesha akiwa amefungwa pingu na kupelekwa gereza la Shala huko El-Fasher. Inajulikana kwamba alifikishwa mbele ya bodi ya nidhamu. Lakini kulingana na shirika la habari la REUTERS, baadaye aliachiliwa kimya kimya na kupelekwa tena kwenye uwanja wa vita.
Kuachiliwa kwake kuliamriwa na kaka yake Hemedti
Pia kulingana na shirika hilo la habari, kaka yake Jenerali Hemedti, Abdel-Rahim Daglo, naibu kamanda wa RSF, ndiye ambaye aliamuru kuachiliwa kwa Abu Lu Lu. REUTERS inaongeza kwamba alirudishwa Kordofan ili kuwakusanya wanajeshi wake, pamoja na maagizo ya kutochapisha tena chochote kwenye mitandao ya kijamii.
Siku ya Jumatatu, Mei 18, msemaji wa Tasis, serikali iliyowekwa na RSF, alikataa kuachiliwa kwa Abu Lu Lu. Msemaji huyo alisema kwamba yeye na makamanda wengine walioshutumiwa kwa ukatili wakati wa vita vya El-Fasher bado wako kizuizini na watahukumiwa na mahakama maalum. “Tasis imejitolea kikamilifu kuwafikisha mbele ya sheria wale waliohusika na uhalifu dhidi ya raia,” msemaji wa Tasis ameongeza.
