Makundi ya timu 48 zitakazoshiriki michuano AFCON 2027 yanajulikana rasmiMakundi ya timu 48 zitakazoshiriki michuano AFCON 2027 yanajulikana rasmi

Droo ya mechi ya michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2027) imefanyika leo Jumanne, Mei 19, jijini Cairo, na Makundi ya timu za soka zitakazoshiriki michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2027 hatimaye yanajulikana.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilifanya droo hiyo mnamo Mei 19, 2026, ambapo timu ziligawanywa katika makundi 12, kila moja likiwa na timu nne.

Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) imeendeshwa na magwiji wanne wa soka wa Afrika: Max-Alain Gradel kutoka Côte d’Ivoire, William Troost-Ekong kutoka Nigeria, Essam El Hadary kutoka Misri, na Trésor Mputu kutokaJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mataifa arobaini na nane yanashiriki katika mechi hizi za kufuzu, ikiwa ni pamoja na nchi mwenyeji Kenya, Tanzania, na Uganda.

Morocco, taifa la Afrika lililo katika nafasi ya juu katika orodha ya FIFA, litakabiliana na Gabon na Niger, miongoni mwa mengine. Misri ya Mohamed Salah itacheza na Angola, Malawi, na Sudan Kusini. Côte d’Ivoire, mabingwa wa Afrika 2023, itakuwa katika kundi moja na Ghana. Senegal itakabiliana na Msumbiji, Sudan, na Ethiopia. Algeria, mabingwa wa Afrika 2019, itakuwa nafasi inayopigiwa upatu dhidi ya Zambia, Togo, na Burundi. Guinea itamenyana na Afrika Kusini kwa nafasi pekee ya kufuzu katika Kundi D, kwani Kenya tayari imefuzu kama taifa mwenyeji.

Mechi hizo zitafanyika katika vipindi vitatu vya FIFA, kati ya mwezi Septemba 2026 na Machi 2027. Timu 48 zimegawanywa katika makundi 12 ya timu nne. Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa mashindano ya mwisho. Katika makundi yenye moja ya mataifa mwenyeji, timu ya ziada pia itapata nafasi katika mashindano.

Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itaanza Jumamosi, Juni 19, 2027, huku fainali ikichezwa Jumamosi, Julai 17, 2027.

Makundi yamepangwa kama ifuatavyo:

Kundi A: Morocco, Gabon, Niger, Lesotho

Kundi B: Misri, Angola, Malawi, Sudan Kusini

Kundi C: Côte d’Ivoire, Ghana, Gambia, Somalia

Kundi D: Afrika Kusini, Guinea, Kenya, Eritrea

Kundi E: DR Congo, Equatorial Guinea, Sierra Leone, Zimbabwe

Kundi F: Burkina Faso, Benin, Mauritania, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kundi G: Cameroon, Comoro, Namibia, Kongo

Kundi H: Tunisia, Uganda, Libya, Botswana

Kundi I: Algeria, Zambia, Togo, Burundi

Kundi J: Senegal, Msumbiji, Sudan, Ethiopia

Kundi K: Mali, Cape Verde, Rwanda, Liberia

Kundi L: Nigeria, Madagascar, Tanzania, Guinea-Bissau

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *