#HABARI: Watumishi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa ku…#HABARI: Watumishi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa ku…

#HABARI: Watumishi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuendesha mafunzo ya elimu ya uraia, utawala bora, na usimamizi wa rasilimali asilia.

Mafunzo hayo, yaliyofunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Katiba, Wakili Prosper Kisinini, yanalenga kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi wa watendaji wa ngazi za chini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mtendaji wa Kijiji cha Nyamalogo, Veronica Joji, alieleza kuwa elimu waliyoipata imewapa uelewa mpana kuhusu uzalendo, uwajibikaji, na misingi ya utawala bora inayotakiwa kuzingatiwa kazini ili kuongeza imani ya wananchi kwa viongozi wao.

Naye Mtendaji wa Kata ya Didia, Husen Majaliwa, alisisitiza kuwa maarifa hayo yatawasaidia kufanya kazi kwa weledi zaidi na aliiomba Serikali kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wengi zaidi wa ngazi za msingi.

Kwa ujumla, washiriki hao wamebainisha kuwa elimu waliyoipata itakuwa chachu ya kuimarisha ulinzi wa mali na rasilimali za taifa, huku ikikuza uwazi na tija katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wamebainisha kuwa hatua hii ni muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii na kuhakikisha kuwa rasilimali asilia zinasimamiwa ipasavyo kwa manufaa ya wananchi wote.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *