Nigeria na Marekani zadai kuwauwa magaidi 175Nigeria na Marekani zadai kuwauwa magaidi 175

Nigeria na Marekani zimedai kutekeleza mashambulio ya pamoja yaliyoua zaidi ya wanajihadi wa kiislamu 175 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, akiwemo kiongozi wa pili wa juu wa kundi la Islamic State.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka makao makuu ya ulinzi nchini Nigeria,operesheni hiyo ya anga na ardhini , ililenga na kuharibu vituo vya ukaguzi vilivyokuwa vimewekwa na wanajihadi hao,silaha,vituo vya kupanga mashambulizi na mtandao wa ufadhili wa ISWAP.

Msemaji wa idara ya ulinzi ,meja jenerali  Samaila Uba,operesheni hizo zinazongozwa na Marekani ni sehemu ya kampeni ya kuwamaliza wanajihadi ambao wamekuwa tishio la kiusalama nchini Nigeria.

Hivi karibuni shambulizi lingine la pamoja lilisababishwa kuwauwa kwa Abu-Bilal al-Minuki kamanda wa pili wa Islamic state, lilikuwa ni ushindi mkubwa kwa serikali ya Nigeria na Washington.

Aidha mwishoni mwa wiki,viongozi wengine wa ISWAP Abd al-Wahhab aliyekuwa akiratibu mashambulizi na propaganda, na Abu Musa al-Mangawi na  Abu al-Muthanna al-Muhajir,ambaye walikuwa wanasimamia habari na washirika wa karibu wa al Minuki.

Kundi la Islamic state linachangia asilimia 86 ya migogoro  katika miezi mitatu ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika la kufuatilia migogoro na mizozo ya silaha. ⁠

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *