Uganda: Watu zaidi ya 100 wamewekwa karatani wakishukiwa kuambukizwa EbolaUganda: Watu zaidi ya 100 wamewekwa karatani wakishukiwa kuambukizwa Ebola

Nchini Uganda, watu zaidi ya 100 wamewekwa karatini, baada ya kushukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola, wakati huu serikali ikiweka mikakati ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo, baada ya watu wawili kuthibitishwa kuambukizwa jijini Kampala.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Serikali Allan Kasujja, amethibitisha watu kadhaa kuwekwa karatani wakiwemo wahudumu wa afya waliotoa matibabu kwa raia DRC ambaye hata hivyo alifariki wiki iliopita baada ya kuambukizwa Ebola.

“Zaidi ya watu mia moja wametambuliwa na wametengwa na wanatibiwa na madaktari wenye uzoefu mkubwa. Uganda imeweza kudhibiti Ebola kwa ufanisi mkubwa hapo awali na tunawaambia watu wawe waangalifu sana.” Amesema Allan Kasujja.

Kufuatia hali hiyo, hatua zimechukuliwa kuzuia uwezekano wa maambukizi ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa lazima katika maeneo ya mpakani na kunawa mikono katika maeneo yenye watu wengi.

Shule zinazotarajiwa kufunguliwa Jumatatu wiki ijayo zimeagizwa kuhakikisha kuna usafi na vipimo vya joto vinachukuliwa.

Wizara ya afya hata hivyo imesema ina uwezo wa kutosha na uzoefu wa kushughulikia mlipuko wowote. Dkt Henry Mwebesa, ni mwenyekiti wa Tume ya Huduma ya Afya

“Tumejenga mfumo imara sana wa kukabiliana na dharura za afya ya umma katika muda wa ziada. Kwa ushirikiano wa Shirika la Afya Ulimwenguni na washirika wengine, tutakabiliana vilivyo na mlipuko huu kwa sababu hapo awali tumekuwa na milipuko na kuidhibiti kwa wakati wa rekodi na kwa viwango vya chini vya vifo vya kesi.”  Amesema Dkt Henry Mwebesa.

Umoja wa Mataifa tayari umetoa Dola za Marekani Milioni 3.5 huku Umoja wa Ulaya ukiongeza Euro Milioni 8 kusaidia juhudi zinazoongozwa na Serikali katika vita dhidi ya Ebola.

Dkt Jane Ruth Achieng ni Waziri wa afya nchini Uganda.

“Hatujawahi kushughulikia mlipuko wowote ambao umetugharimu chini ya Dola za Kimarekani milioni 50. Kawaida hufikia Dola milioni 150 hadi 200 kwa sababu ya mambo mengi tunayopaswa kufanya.” Ameeleza Dkt Jane Ruth Achieng.

Wizara ya afya inasema imerikodi va viwili vya Ebola kutoka inje ya inchi. Mtu mmoja amefariki huku mmoja akiendelea na matibabu katika hospitali kuu ya Mulago hapa mji wa Kampala.

Kenneth Lukwago, Kampala, RFI Kiswahili 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *