#HABARI:David Djumbe, Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akionyesha mikono yake ilivyoathirika baada ya kufungwa pingu na watu wasiojulikana.
Djumbe yupo kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam kwa mahojiano, kuanzia saa sita mchana wa leo Alhamisi, Mei 21, 2026. Kituoni hapo Jumbe alikuwa na rafiki yake Allan Macha ambaye walikuwa pamoja wakati akichukuliwa na watu wasiojulikana.
Pamoja na mambo mengine Jumbe amefika kituoni hapo kufunguliwa pingu.
Pingu hizo Djumbe alifungwa na watu wanaodaiwa kumteka usiku wa kuamkia leo Alhamisi, maeneo ya nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kutoroka nazo.
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imeeleza kuwa inafuatilia tukio hilo.

(Feed generated with FetchRSS)
