
Sierra Leone imekuwa taifa jingine la Afrika kuwapokea wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump na kampeni yake dhidi ya aliowataja wahamiaji haramu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa mamlaka za nchi hiyo, ndege ya kwanza iliyokuwa na wahamiaji 9 ilitua majira ya asubuhi katika uwanja wa ndege ulioko nje kidogo ya jiji kuu Freetown.
Waziri wa mambo ya nje Timothy Musa, amethibitisha kupokea kundi hilo la kwanza la wahamiji 9 kati ya 25 wanaotarajiwa kupokelewa na nchi hiyo, wengi wakiwa ni raia wa Nigeria, Ghana, Guinea na Senegal.
Maofisa wa afya nchini Sierra Leone, wamesema wahamiaji hao ambao 7 walikuwa wanaume na wawili wanawake, wanafanyiwa uchunguzi na kupewa msaada wa kisaikolojia, kutokana na kuathirika baada ya kuzuiliwa kwa muda mrefu na mamlaka za Marekani.
Kwa mujibu wa Serikali, wahamiaji hao wanatarajiwa kurejeshwa kwenye nchi zao za asili ndani ya majuma mawili yajayo.
