Wanafunzi wa kigeni ambao si raia wa EU kulipa ada kubwa katika vio vikuu nchini UfaransaWanafunzi wa kigeni ambao si raia wa EU kulipa ada kubwa katika vio vikuu nchini Ufaransa

Kusoma nchini Ufaransa kutakuwa ghali zaidi kwa wanafunzi ambao si raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kulingana na amri kutoka Wizara ya Elimu ya Juu ya Ufaransa iliyotolewa siku ya Jumatano, Mei 20, 2026, wengi wa wanafunzi hawa wasio wa Ulaya watalazimika kulipa ada ya masomo ya juu zaidi kuanzia mwaka ujao wa masomo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Karibu euro 3,000 kwa mwaka kwa shahada ya kwanza, ikilinganishwa na euro 178 leo: hivyo ndivyo ada ya masomo katika chuo kikuu cha Ufaransa itakavyowagharimu wanafunzi wasio wa Ulaya. Amri hii ilichapishwa kama sehemu ya mpango mpya unaoitwa “Choose France For Higher Education” na Waziri wa Elimu ya Juu, Philippe Baptiste, ambaye alitangaza Aprili 20 nia yake ya kutekeleza kikamilifu ada tofauti za masomo kwa wanafunzi wasitoka nchi wanachama wa EU katika vyuo vikuu vya Ufaransa. Hatua hii imekuwepo tangu mwaka 2019 lakini haijatumika sana hadi sasa.

Kwa hivyo serikali imeamua kuweka sheria kali zaidi: vyuo vikuu, ambavyo vitapunguza ada hii, vitajikuta matatani na kuanza kuchukuliwa hatua kali hususan kupunguziwa misamaha ya kulipa kodi kwa 20% ifikapo Septemba 2028. Ni wanafunzi pekee ambao tayari wamejiandikisha katika kozi ya masomo watakaoweza kuendelea kunufaika na malipo yao ya sasa.

Kwa Waziri wa Elimu ya Juu, lengo ni kuvutia wanafunzi wenye uwezo mkubwa, wakifuata mfumo wa Anglo-Saxon. Badala yake, Ufaransa inaahidi kurahisisha kupata visa za kazi baada ya masomo. Mbinu hii inavutia kifedha kwa serikali, lakini vyama vya wafanyakazi vinaiona kuwa si ya haki na isiyolingana.

Baada ya maandamano ya awali mnamo Mei 12, muungano wa vyama vya wafanyakazi umeitisha siku nyingine ya maandamano mnamo Mei 26 ili kuishinikiza serikali irejelee hatua hii, ambayo vyama vya wafanyakazi vinaiona kuwa “haifai na imepitwa na wakati.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *