#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kigoma, imefanikiwa kuokoa milioni kumi na saba, kutoka kwa…#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kigoma, imefanikiwa kuokoa milioni kumi na saba, kutoka kwa…

#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kigoma, imefanikiwa kuokoa milioni kumi na saba, kutoka kwa viongozi wa Kijiji cha Mgambazi wilayani uvinza, waliokuwa wanataka Bw. Paskali Donadi Lala na familia yake, kulipa fedha hizo kama faini halali katika serikali ya Kijiji kwa kosa la kufugia Ngo’ombe ndani ya eneo la hifadhi kinyume na utaratibu.

Hali hiyo inamfanya Lala kugoma kulipa fedha hizo, na kuwasilisha taarifa hiyo katika ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Uvinza na kuchukua hatua ya ufatiliaji, ndipo ilibainika kiasi kilichotakiwa kulipwa kwa kila ng’ombe ni shilingi elfu 500, hivyo kufaya kiasi cha faini halali kuwa shilingi milioni moja na elfu ishirinitu.

Ikumbukwe kuwa awali kiasi cha shilingi milioni kumi na saba, viongozi wa Kijiji walitaka wana Lala awape fedha mkononi, ambapo huenda wangezipiga nje ya utalatibu wa Serikali, na kiasi kilicholipwa kisheria ni kiasi cha milioni moja na elfu ishirini, katika akaunti ya Serikali ya Kijiji cha Mgambazi na sio fedha Taslim.

Kutokana na hatua hiyo, Bwana Paskali Donadi Lala amepongeza TAKUKURU kwa kuingilia kati suala hilo, ambalo lingemghalimu kulipa fedha nyingi na nje ya utalatibu wa serikali na kunufaisha viongozi wa Kijiji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *