Adeyum asaka rekodi mpya Bigman FCAdeyum asaka rekodi mpya Bigman FC

BAADA ya beki wa kushoto wa Bigman FC, Adeyum Saleh kufikisha mabao matano msimu huu, nyota huyo amebakisha bao moja ili aweke rekodi mpya ya kufunga mengi zaidi katika timu hiyo, tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita wa 2024-2025.

Mabao matano aliyofunga beki huyo msimu huu ni sawa na ya Mnigeria Collins Kelvin Nwobodo ambao wote wanahitaji kufunga bao moja ili kuvuka rekodi ya msimu uliopita, ambao Ally Ally na Emmanuel Nyonyi waliifungia timu hiyo pia mabao matano.

Ally Ally anayechezea msimu akiwa na Geita Gold na Emmanuel Nyonyi anayekipiga katika kikosi cha Mbeya Kwanza, ndiye mmoja wa wachezaji waliofunga mabao mengi msimu uliopita baada ya kuifungia Bigman matano, rekodi inayoweza kuvunjwa na Adeyum au Collins.

ADEY 01

Akizungumzia kiwango chake msimu huu, nyota huyo aliyewahi kuwika na timu mbalimbali zikiwemo Yanga, Coastal Union, Stand United, Kagera Sugar na Dodoma Jiji, amesema atapambana na ikiwezekana aandike rekodi yake mpya kikosini humo.

ADEY 02

“Licha ya kucheza beki ila nimekuwa huru sana uwanajani kutokana na aina ya uchezaji wetu, jambo linalonipa nafasi nzuri ya kufunga zaidi mabao, malengo yangu kijumla ni kuona timu inafanya vizuri na mimi binafsi,” amesema Adeyum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *