Kwa muda sasa, biashara ya dawa zinazodai kuongeza nguvu za kiume imekuwa ikikua kwa kasi kubwa mitandaoni, madukani na hata kwa…Kwa muda sasa, biashara ya dawa zinazodai kuongeza nguvu za kiume imekuwa ikikua kwa kasi kubwa mitandaoni, madukani na hata kwa…

Kwa muda sasa, biashara ya dawa zinazodai kuongeza nguvu za kiume imekuwa ikikua kwa kasi kubwa mitandaoni, madukani na hata kwa wauzaji wa mtaani. Kila kona kuna matangazo yanayoahidi matokeo ya haraka; kuongeza uwezo ndani ya dakika chache au kurejesha uimara wa mwanaume.

Kwa wengi, hii huonekana kama huduma inayojibu mahitaji ya jamii. Lakini nyuma ya biashara hiyo kuna simulizi la hofu, shinikizo la kijamii pamoja na uelewa usio sahihi wa afya ya mwanaume. Jamii imejengewa fikra kwamba wanaume wengi wanapitia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, hali inayofanya hata changamoto za kawaida kuonekana kama matatizo makubwa ya kiafya.

Mwanaume anapoanza kuamini kuwa ana changamoto hiyo, hata kama hana tatizo la moja kwa moja, hujikuta akitafuta suluhisho la haraka. Katika mazingira ambayo mazungumzo ya afya ya uzazi kwa wanaume bado yanafanyika kwa siri au aibu, wengi hukimbilia kutumia dawa kabla ya kupata uchunguzi wa kitaalamu.

Wapo wanaotumia bidhaa bila kujua viambata vyake, zimetengenezwa wapi au kama zimeidhinishwa. Hali hii inaweza kuwa hatari zaidi kwa watu wenye magonjwa kama presha, kisukari au matatizo ya moyo.

Kadri matumizi yanavyoendelea, baadhi ya wanaume huanza kujenga utegemezi wa kisaikolojia wakiamini uwezo wao unategemea dawa badala ya afya ya mwili na akili. Hapo ndipo tatizo linapokuwa kubwa zaidi, kwani si kila changamoto ya muda inahitaji dawa. Mara nyingi kinachohitajika ni uchunguzi, kupunguza msongo wa mawazo, kuboresha usingizi, kufanya mazoezi na kudhibiti magonjwa sugu.

Kwa upande mwingine, jamii nayo imechangia. Mwanaume amefundishwa kuwa lazima awe imara kila wakati, asiombe msaada wala kuonyesha udhaifu. Matokeo yake changamoto za afya ya uzazi hubaki gizani huku soko la “suluhisho za haraka” likiendelea kukua.

Daktari wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Mussa Msemo anaeleza kuwa matumizi ya vitu visivyo tiba halisi yanaweza kuharibu afya ya uzazi na kuongeza hatari ya magonjwa mengine kutokana na uwezekano wa kuchanganywa na kemikali hatarishi.

✍Halima Abdallah
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *