
Serikali mpya ambayo imetangazwa saa chache tu baada ya sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule, ina wajumbe 24, wakiwemo mawaziri kadhaa wa zamani waliohudumu katika utawala wa Talon. Ingawa robo ya nafasi hizo zinashikiliwa na wanawake, hakuna viongozi wa upinzani waliojiunga na rais Romuald Wadagni wakati wa kampeni ambao wamejumuishwa katika serikali hiyo mpya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Cotonou, Jean-Luc Aplogan
Nchini Benin, baada ya kuapishwa, rais mteule wa Benin, Romuald Wadagni, alitangaza muundo wa serikali yake ya kwanza jioni ya Jumapili, Mei 24.
Ikiwa na wanachama 24, inajumuisha viongozi wapya lakini pia inategemea mawaziri wa zamani waliohudumu katika utawala wa Talon, kwani takriban theluthi moja ya wale waliohudumu katika serikali inayomaliza muda wake ya mkuu wa nchi anayeondoka wamejumuishwa katika timu hii mpya. Ingawa baadhi wameeendelea kushikilia nyadhifa zao, wengine wamejikuta wakibadilishiwa nyadhifa zao.
Robo ya nafasi hizo zinashikiliwa na wanawake
Kwa mfano, hivi ndivyo ilivyo kwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Benin Olushegun Adjadi Bakari, ambaye anakuwa Waziri wa Utalii na Biashara ya Nje, mwenye dhamana ya viwanda na uendelezaji wa uwekezaji binafsi. Wizara ya Mambo ya Nje, ambayo hapo awali alisimamia, sasa inaongozwa na balozi wa Benin huko Paris, Corinne Brunet, huku wizara ya Ulinzi na Usalama zikiwekwa chini ya mamlaka ya moja kwa moja ya Mkuu wa Nchi, ambaye alikuwa amezipa kipaumbele katika kampeni yake.
Nafasi inayotarajiwa sana ya Waziri wa Uchumi na Fedha, ambayo hapo awali ilikuwa ikishikiliwa na Romuald Wadagni mwenyewe, inashikiliwa na Mkurugenzi wake Mkuu wa zamani wa Uchumi, Aristide Médenou, ambaye atasaidiwa na manaibu waziri watatu.
Ingawa robo ya nafasi katika serikali hii mpya zinashikiliwa na wanawake, hakuna watu wa upinzani waliojiunga na mgombea wakati wa kampeni waliojumuishwa katika serikali hii mpya. Mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri utafanyika Jumatano, Mei 27.
