El Baradei: Mwendawazimu Trump anatafuta njia ya kujiondoa kwenye vita dhidi ya IranEl Baradei: Mwendawazimu Trump anatafuta njia ya kujiondoa kwenye vita dhidi ya Iran

Mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametangaza kuwa mtu mmoja mwendawazimu alianzisha vita dhidi ya Iran na sasa anatafuta njia ya kujiondoa vitani.

Akizungumzia juhudi za kufikia makubaliano ya kukomesha vita vya kikatili vya Israel na Marekani dhidi ya Iran, Mohamed El Baradei, mkuu wa zamani wa Wakala wa Kimataifa na Nishati ya Atomiki, ameandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Vita hivi vya kikatili vilianzishwa kwa mara ya pili na mtu mwendawazimu (Trump) na mwenzake anayetafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (Netanyahu).

El Baradei amesisitiza kwamba sasa kiongozi wa vita hivyo vya kichokozi anajaribu kutafuta njia ya kujiondoa vitani na anapiga simu kwa serikali za nchi za kikanda ili kujenga hisia kwamba hivi vilikuwa vita ya kikanda kati yao na Iran, huku nchi hizo zikiwa hazijui lolote kuhusu vita hivi hadi pale baadhi ya miale yake ilipozikumba!

“Ni kipindi cha udanganyifu, unafiki na fedheha…” amesema El Baradae ambaye amekuwa akikosoa sana misimamo ya kinafiki na ya kuchochea vita ya nchi za Magharibi dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *