Rais wa Nigeria Tinubu kugombea tena kiti cha urais baada ya kuteuliwa na chamaRais wa Nigeria Tinubu kugombea tena kiti cha urais baada ya kuteuliwa na chama

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, atagombea tena katika uchaguzi mkuu mwezi Januari mwakani baada ya kushinda uteuzi wa chama chake katika kura za mchujo za All Progressives Congress.

Baada ya kuvuka utaratibu wa kura za mchujo za chama chake cha All Progressives Congress (APC), Tinubu atateuliwa kuwa mgombea wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais cha 2027.

Baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2023, Tinubu hajawahi kuficha azma yake ya kuhudumu kwa muhula wa pili wa miaka minne.

Ushindi wake ulitangazwa huku chama cha APC kikisifu mchakato huo kama uthibitisho wa demokrasia ya ndani. Tinubu alikabiliana na mfanyabiashara asiyejulikana, Stanley Osifo, ambaye alitumia naira milioni 100 (karibu dola 73,000) kwa ajili ya kupata haki ya kusimama dhidi ya rais.

Tinubu ndiye anayetazamiwa kushinda uchaguzi wa Januari 2027, kutokana na upinzani dhaifu na uliogawanyika.

Chama chake cha APC kinadhibiti majimbo 31 kati ya 36 nchini Nigeria, kutoka majibo 21 mwaka wa 2023.

Katika muhula wake wa kwanza, Tinubu amepitisha mageuzi mbalimbali yaliyokusudiwa kukuza uchumi na kujenga imani ya wawekezaji wa kimataifa.

Hata hivyo Wanigeria wengi wa kawaida wana mtazamo mbaya kuhusiana na uchumi.

Mfumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 30 mwaka wa 2024 na uliendelea kuwa wa asilimia 15 mwanzoni mwa mwaka huu 2026, huku bei ya mafuta ikiongezeka mara nne katika kipindi cha miaka minne. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia karibu asilimia 60 ya Wanigeria wanaishi katika umaskini, likiwa ni ongezeko la asilimia nne tangu wakati Tinubu alipochukua madaraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *