Mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Ibrahim Rabhi, amesema maslahi binafsi ya pande zinazohusika ni miongoni mwa vikwazo vinavyochelewesha kufikiwa kwa makubaliano kati ya Iran na Marekani.
Rabhi ameeleza kuwa kila upande unatanguliza manufaa ya taifa lake, hali inayofanya kuwa vigumu kufikia muafaka wa haraka katika mzozo huo.
Hata hivyo, amesema licha ya changamoto hizo, bado kuna dalili za matumaini kufikiwa kwa suluhu, kufuatia juhudi za upatanishi zinazoendelea kufanywa na baadhi ya nchi.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
(Feed generated with FetchRSS)
