Baqaei: Marekani inapasa kudhamini ushiriki wa timu ya taifa ya Iran katika mashindano ya Kombe la DuniaBaqaei: Marekani inapasa kudhamini ushiriki wa timu ya taifa ya Iran katika mashindano ya Kombe la Dunia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia uvumi unaoendelea kuhusu kushiriki wa timu ya taifa ya kandanda ya Iran katika Kombe la Dunia la FIFA la 2026, na kusisitiza kuwa Marekani inawajibika kuandaa mazingira yanayofaa kwa timu hiyo kushiriki katika mashindano bila vizuizi vyovyote.

Ismail Baqaei ameeleza haya katika mkutano wa kila wiki na vyombo vya habari baada ya kusambaa ripoti kwamba Shirikisho la Soka la Iran chini ya uongozi wa Mehdi Taj, limeamua kuhamisha kambi ya mazoezi ya timu hiyo kutoka Marekani hadi Mexico kutokana na matatizo ya mara kwa mara ya upataji viza ya Marekani.

Alipoulizwa iwapo FIFA inaweza kukabiliana ipasavyo na ukwamishaji wowote wa Marekani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Kwa kuzingatia kuwa FIFA ni kituo kikuu cha mawasiliano kwa ajili ya misaada ya kilojistiki katika mashindano hayo ya dunia, Marekani pia ina wajibu kama nchi mwenyeji mwenza.

Ameongeza kuwa, Marekani ina wajibu wa kuandaa mazingira yote yanayojitajika kwa ajili ya Timu ya Taifa ya Iran ya Soka ili iweze kushiriki bila ukwamishaji au kizuizi chochote.

Amefafanua kuwa, uamuzi wa kuhamisha kambi ya mazoezi  ya Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Iran umefanywa kwa uratibu kamili na FIFA, Shirikisho la Soka la Mexico, na wadau husika wa Marekani ili kutatua ukamishwaji unaoweza kujitokeza.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *