JKT yazinduka BDLJKT yazinduka BDL

JKT imezinduka katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL), baada ya kuifunga Veins BC kwa pointi 57-56 kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga.

Katika mechi ya kwanza, JKT ilifungwa na Stein Warriors pointi 70-52, kabla ya kufungwa na ABC 70-68.

Charles Makene, mchezaji wa zamani wa JKT na timu ya Taifa, amesema timu yake ilipoteza mechi hizo kutokana na makosa madogo ambayo yalirekebishwa wakati wa mazoezi.

Makene ambaye ni meneja wa timu ya wanawake JKT Stars , amewataka  wapenzi wa timu hiyo  wafike uwanjani kuiona ikicheza.

“JKT ilipoteza mechi ya kwanza katika robo ya nne baada ya Stein Warriors kufunga pointi 21, iliyoiwezesha kushinda pointi 70-52, kabla pointi hizo kufungwa tulikuwa tunaongoza kwa pointi 45-40,” alisema Makene.

Katika mechi ya pili dhidi ya ABC, ilipoteza baada ya wachezaji wake kujisahau.

“Unajua JKT inaundwa na wachezaji waliokuzwa katika  kambi ya JKT, hivyo kadri ligi inavyoendelea wamekuwa wakibadilika,” alisema Makene.

Katika fainali ya Ligi ya BDL iliyofanyika mwaka jana, ilifungwa na  Dar City  katika michezo 2-0.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *