Kenya: Jiji la Mombasa lakabiliwa na tatizo la magenge ya kihalifuKenya: Jiji la Mombasa lakabiliwa na tatizo la magenge ya kihalifu

Jiji la Mombasa, ambalo ni kitovu kikuu cha utalii katika pwani ya Kenya, siku za hivi karibuni limeendelea kushuhudia ongezeko la utovu wa usalama kutokana na kuwepo kwa magenge ya uhalifu katika mitaa kama Kisauni, Nyali na Likoni.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wafanyabiashara sasa hufunga biashara zao mapema kwa hofu ya kushambuliwa.

Ken, si jina lake halisi, ni mmoja wa waliowahi kuwa mwanachama wa genge la uhalifu jijini Mombasa lakini ameachana na uhalifu.

“Nimeachana na mambo ya uraibu. ” Alisema Ken, aliachana na uhalifu.

Abdhallah Abdulrahman, kiongozi wa jamii katika eneo la Kisimani huko Nyali, anasema kukosekana kwa ukaribu kati ya wazazi na watoto pamoja na matumizi ya vijana katika siasa mbaya pia imechangia ongezeko la makundi hayo.

“Wazazi wao wanajiweza lakini wanashindwa kuwapa watoto wao malezi mazuri. ” Alisema Abdhallah Abdulrahman, kiongozi wa jamii.

Kwa upande wake, Walid Kassim, mkurugenzi mkuu wa asasi ya kijamii ya Muhuri, amesema suluhisho linahitaji ushirikishwaji  zaidi wa vijana katika mipango ya maendeleo na maamuzi ya umma.

“Vijana wetu hawashirikishwi kwenye meza ya maamuzi utapata wazee, asasi tofauti zimeketi kushauriana ni vipi watadhibiti usalama. ” Alisema Walid Kassim, mkurugenzi mkuu wa asasi ya kijamii ya Muhuri.

Shaaban Mwalimu, mchambuzi wa masuala ya usalama, anaeleza ni kwa nini kuna ongezeko la visa vya uhalifu jijini Mombasa.

“Eneo hili limekuwa likijihisi kwamba limetengwa kwa siku nyingi, umaskini na kutengwa kisiasa.” Alieleza Shaaban Mwalimu, mchambuzi wa masuala ya usalama.

Wadau wa utalii wanaonya kuwa hali ya usalama ikizidi kuzorota inaweza kuathiri sekta ya utalii katika mji huu ambao unategemea wageni kutoka ndani na nje ya nchi, huku serikali ikisema, haitafanya mazungumzo na magenge ya kihalifu na watuhumiwa wanapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Diana Wanyonyi, Mombasa RFI –Kiswahili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *